Dar City balaa, inatupia tu BDL

WAKATI Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) upandae wa wanaume ikiendelea, imeonyesha timu ya Dar City inaongoza kwa kufunga ponti 1786.

Pointi hizo zimepatikana kutokana na michezo 21 iliyochezwa ikifuatiwa DB Oratory iliyofunga 1387, Vijana ‘City Bulls’ (1372), Savio  (1357), Mchenga Star (1343), UDSM Outsiders (1231), Srelio (1231) na Pazi (1205).

Zingine ni Ukonga Kings (1191), KIUT (1087), ABC (1059), Crows (1014), Jogoo (1007), Chui 919 na Mgulani JKT (871) Wakati huohuo mchezo noamba 335 kati Tausi Royals na DB Lioness na 351 kati ya timu ya DB Lioness na Kurasini Divas umeahirishwa.

Taarifa iliyotolewa na kamati ya ufundi ya mashindano hayo imeeleza kwamba kuahirishwa kumetokana na wachezaji  sita wa DB Lioness kwenda katika majukumu mengine ya kimichezo. Kifungu cha .4:8 kinarusuhu kuahirishwa michezo ya timu kama kuna sababu zinazojitosheleza.

Related Posts