DC Sweda atoa wito serikali kuiwezesha taasisi ya afya inayotengeza bidhaa za maabara

Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Juma Sweda ametoa wito kwa serikali kuisadia taasisi ya mafunzo ya afya Lugarawa (LUHETI) ikiwemo kutoa mkopo ili kuinua na kukuza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na taasisi hiyo na kuishia kwenye mafunzo pekee ya wanafunzi waliopo kwenye taasisi hiyo badala ya kusambazwa na kuwafikia watumiaji wengine kutokana na ujuzi mkubwa unaofanywa katika taasisi.

Sweda ametoa wito huo kwa serikali ya wilaya ya Ludewa alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka mahafali ya ya 24 ya wahitimu 323 wa taasisi ya mafunzo ya afya Lugarawa (LUHETI) iliyopo wilayani Ludewa ambapo amesema taasisi hiyo imeonyesha uwezo mkubwa wa kutengeneza Ontiments,creams,paste na gels kwa ajili ya kupakaa nje ya mwili wa binadamu huku pia wakitengeneza bidha nyingine kama Paracetamol syrup,mixtures na lotions ambazo zimekuwa zikitumiwa kwa mafunzo kwa wanafunzi katika taasisi.

“Wanaweza kutengeneza bidhaa ambayo wanaweza kuiuza kwenye nchi yetu,serikali tuna uwezo wa kutoa mpaka mikopo kwa vijana kwa hiyo kama vijana kushirikiana na kanisa tukianzisha hicho kitu hapa na vijana wakaendelea kulelewa hapa na kuwaletea fedha naamini wataweza kutengeneza hizi bidhaa ambazo pia wataweza kutuuzia serikali na hivyo tutakuwa tumewasaidia wao lakini tumeisadia nchi tena”amesema Sweda

Vile vile amebainisha kuwa kutokana na uwezo huo itasadia kuto agiza kila bidhaa nje ya nchi ambapo ametoa rai kwa mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa kulifanyia kazi jambo hilo litakalokwenda kupunguza mzigo wa serikali lakini pia kuikomboa sekta ya afya.

Naye Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe Padre Eusebio Samwel Kyando,amesema kanisa hilo litaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha Mtanzania anaendelea kupata huduma safi ya afya na elimu ili kuondoa changamoto ya ujinga na maradhi kwa watanzania.

“Lengo letu la msingi ni kuhudumia watu wote tunalenga jambo moja kuhakikisha jambo moja kwamba Mtanzania anapata huduma safi ya afya na elimu na hatuwezi kuwa na shida nyingine,wote tunaelekea huko tuwahudumie watanzania waweze kupata huduma nzuri ya afya lakini pia na elimu kuondoa ujinga lakini pia maradhi kwa hiyo sisi hatufanyi kazi hii kama washindani sisi ni wadau washiriki pamoja na serikali yetu kwa ajili ya kuwakwamua wananchi”amesema Askofu Kyando.

Kwa upande wake Buteye Dotto Buteye ambaye ni mkuu wa taasisi hiyo ya mafunzo ameiomba serikali kutazama na kutanua wigo katika kozi zingine za afya kwa kuwapa mikopo wanafunzi ili waweze kulipa ada kwa kuwa zipo familia zingine ambazo wamekuwa wakishindwa kulipia karo.

Albert Ndetije na Brenda Shayo ni miongoni mwa wahitimu katika taasisi ya LUHET wanasema zipo changamoto nyingi wanazopitia vyuo vya kati kwenye upande wa ada na kusababisha wanafunzi wengi kusitisha masomo yao na kuiomba serikali kuona umuhimu wa kuongeza kozi zingine pia kwenye utoaji wa mikopo kwa wanafunzi ili waweze kufanikisha ndoto zao katika elimu.

Related Posts