Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Kisheria yaja na Suluhu ya migogoro ya Ardhi na Miradhi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Eliakimu Maswi akizungumza kuhusiana na mafanikio ya Kampeni Msaada wa Huduma za Kisheria ya Mama Samia wakati alipotembelea Banda la Katiba na Sheria katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Katiba na Sheria Eliakimu Maswi amesema kuwa tangu walipoanza Kampeni ya Msaada wa Hudama za Kisheria ya Mama Samia wahitaji wengi katika huduma hiyo ni katika miradhi pamoja na ardhi.
Amesema katika miradhi wanaofika kuhitaji msaada huduma za Kisheria ni wanawake hiyo ni kutokana desturi za nchi za Afrika.
Hayo aliyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Eliakimu Maswi wakati alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema kuwa katika Viwanja vya Nane Nane Agasti 6 kuanzia asubuhi hadi mchana wamepokea wananchi 397 hiyo inaonyesha uhitaji ni mkubwa na kazi yao walioajiriwa nayo kuhudumia wananchi.
Aidha amesema kuwa wanashukuru kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kukubali jina lake kutumika katika Kampeni hiyo.
Maswi amesema kuwa katika kampeni hiyo wameshatoa huduma za Msaada wa Kisheria katika Mikoa Saba.
“Kama Wizara tumejipanga katika kuwahudumia wananchi katika kupata haki za Kisheria”. amesema Maswi.

Related Posts