KIWANDA CHA SIGARA CHA SERENGETI KUTOA AJIRA ZAIDI YA 12,000 – MOROGORO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kiwanda cha kutengeneza sigara cha Serengeti kilichopo Mkoani Morogoro kitatoa ajira zaidi ya elfu 12,000 kwa wakazi wa Mkoa huo baada ya ujenzi wake kukamilika.

 

 

 

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo Agosti 06, 2024 wakati akizungumza na Wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kiwanda cha kutengeneza sigara cha Serengeti Cigarette Company na upanuzi wa kiwanda cha uchakataji wa tumbaku cha Mkwawa Tobacco Leaf Processors LTD vilivyopo Mkoa wa Morogoro.

 

 

 

Rais Dkt. Samia amesema kuwa kwa sasa kiwanda hicho kina ajira zaidi ya 7,000 ambapo bado hakijakamilika hivyo baada ya ujenzi wake kukamilika kitatoa ajira nyingi zaidi kwa wakazi wa maeneo hayo.

 

 

 

Ikumbukwe kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea na ziara ya kikazi ya siku sita Mkoani Morogoro huku akiendelea kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa huo.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kiwanda cha Sigara cha Serengeti (SCC) katika eneo la Kiwanda cha uchakataji tumbaku Mkwawa (MTPL) Mkoani Morogoro tarehe 06 Agosti, 2024.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mmiliki na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha uchakataji tumbaku Mkwawa (MTPL) na Kiwanda cha Sigara cha Serengeti (SCC) Ahmed Huwel kuhusu taarifa ya mradi wa upanuzi wa Viwanda hivyo Mkoani Morogoro tarehe 06 Agosti, 2024.

Related Posts