KOCHA SIMBA ATUMA SALAM YANGA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

UKISEMA ametuma salam kwa Yanga utakuwa sahihi baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids kusema anaamini kikosi chake kitapata mafanikio makubwa msimu ujao wa 2024/25.

 

 

Simba inayonolewa na Fadlu kwa mara ya kwanza siku ya Simba Day ilionekana hadharani ikicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya APR FC baada ya kurejea nchini Tanzania wakitokea Misri walipoweka kambi kujiandaa na msimu ujao.

 

 

Katika mchezo huo, Kikosi hicho cha Wekundu hao wa Msimbazi kiliibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku kikionyesha soka la kitabuni, mabao yakifungwa na Debora Fernandez pamoja na Edward Balua, na kuwafanya Mashabiki kuamini kuwa, Msimu ujao Wapinzani wataisoma namba.

 

 

Baada ya ushindi huo, sasa Wekundu hao wa Msimbazi wanaelekeza nguvu zao mchezo wa Nusu Fainali Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, ambapo Kocha Fadlu amesema anaamini watapata matokeo mazuri.

 

 

Fadlu amesema kadri siku zinavyokwenda kikosi chake kinakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji akitolea mfano Michezo ya Kirafiki waliyocheza Misri na ule dhidi ya APR ambayo yote Mnyama alishinda. “Bado naendelea kusuka kikosi imara kuelekea msimu ujao. Matarajio yangu na timu kwa ujumla ni kuchukua makombe msimu ujao lakini hilo litawezekana kama tutaunganisha nguvu ya pamoja kuanzia kwa Benchi la ufundi, Wachezaji na hata mashabiki wetu.

 

 

“Nimefurahishwa na sapoti kubwa ya Mashabiki niliyoiona kwenye Tamasha la Simba Day, niseme tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa Ngao ya Jamii (dhidi ya Yanga), hizi siku chache zikizobakia nitaendelea kuyafanyia kazi mapungufu niliyoyaona hii michezo yetu ya kirafiki,” amesema Fadlu.

Related Posts