TFRA yawafikia Wakulima Milioni Nne katika msimu wa Kilimo 2023/2024

Meneja wa Ukaguzi wa TFRA Dkt.Asheri Kalala akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na ukaguzi wa Mbolea katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Meneja wa Usajili na Leseni wa TFRA , Mwahija Irika akizungumza kuhusiana na  upatikanaji wa Mbolea kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

*Yataka wakulima kutembelea Banda la TFRA kupata elimu ya Mbolea nchini

Na Chalila Kibuda, Michuzi Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania amesema kuwa imewafikia wakulima Milioni Nne na mwitikio katika kujua hali ya mbolea nchini utakapoaza Msimu wa Kilimo kwa mwaka 2023/2024.

Akizungumza katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma Meneja Usajili na Leseni wa TFRA Mwahija Irika amesema kuwa wamejipanga msimu wa Kilimo namna watavyoweza kuhakikisha Wakulima wanapata Mbolea.

Amesema kuwa katika msimu huo wakulima wafuate taratibu zilizowekwa katika kupata Mbolea ya ruzuku.

Amesema kuwa mwitikio huo mzuri kwani kama wadhibiti mbolea ni wajibu kutoa majawabu ya kuwatoa hofu juu ya suala la mbolea.

Amesema kuwa moja ya swali linaloulizwa ni suala la mbolea ya Ruzuku ambapo kazi yao ni kuendelea kutoa utaratibu utaotumika katika kupata mbolea kwa bei nafuu kutokana na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu kuona namna bora ya kusaidia wakulima ili kuzalisha chakula kwa wingi.

Hata hivyo amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa ruzuku hiyo kutokana na mahitaji ya wakulima wakati wa msimu wa kilimo utakapoanza.

“Tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi wetu katika kuondoa changamoto wakati wa msimu wa kilimo utakapofika kwa kuweka uwazi wa mbolea ya ruzuku.” amesema

Meneja Ukaguzi wa TFRA Dkt Asheri Kalala amesema wanaendelea na udhibiti na ukaguzi wa Mbolea katika kuhakikisha wananchi wanapata mbolea bora.

Amesema TFRA imekuwa inafanya ukaguzi kwa waagizaji wa mbolea katika kila msimu wa Kilimo na kuwataka kufuata sheria.

Related Posts