Timu za Ligi Kuu Bara kutumia viwanja vya Zanzibar

Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Almas Kasongo amesema kuanzia msimu ujao wa Ligi 2024/25 ni ruksa kwa timu ya Ligi Kuu Bara kutumia viwanja vya Zanzibar.

Kasongo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria semina inayoendeshwa na bodi hiyo.

Kasongo amesema katika kanuni iliyofanyiwa mmaboresho kuelekea msimu mpya ni hiyo ya matumizi ya viwanja Zanzibar kwenye Ligi Kuu.

“Katikati ya msimu ofisi yangu illipokea ombi la timu ya Simba kwenda kutumia uwanja wa New Aman Complex kwaajili ya Ligi Kuu, lakini haikuwezekana kwasabu ya kanuni japo hoja zao zilikuwa na mashiko”

“Tulikaa na Kamati tendaji ya TFF na tukaona hakuna sababu ya kuzuia Hilo na tukaona ni vyema kanuni hiyo ianze kutumika msimu ujao 2024/25″ Alisema Kasongo

Kasongo amesema hayo leo Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria semina inayoondeshwa na bodi hiyo

Wakati huo huo Kasongo amesema ndani ya siku mbili umma utafahamu ratiba na maboresho ya Ligi Kuu Bara 2024/25.

“Ratiba ya ligi pamoja na maboresho ya kanuni zipo tayari na ndani ya siku hizi mbili ofisa habari wa ligi ataweka hadharani.”

“Ni kweli tulikuwa kimya kwa muda mrefu, lakini kimya kirefu kina mshindo, hivyo tunaamini ratiba ya msimu huu itakuwa bora,” alisema Kasongo.

Msimu wa Ligi Kuu Bara 2024/25 utaanza rasmi Agosti 16.

Related Posts