WAKANDARASI WAZAWA KUPEWA KIPAUMBELE MIRADI YA UKUZAJI UCHUMI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema Serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana na Wakandarasi Wazawa kwenye Miradi mbalimbali ya Ujenzi hususani ile inayolenga Maendeleo na ukuaji wa Uchumi dhamira ikiwa ni Kuijenga Tanzania kupitia miradi ya Kimkakati.

 

 

 

Mhandisi Kasekenya ametoa kauli hiyo leo Agosti 06, 2024 Jijini Dar es Salaam kwenye Uzinduzi wa maboresho ya huduma za Benki kwa Wakandarasi, ambapo amewahimiza Makandarasi Wazawa Kuchangamkia Fursa za mikopo zinazotolewa na Taasisi za Kifedha nchini.

 

 

 

“Hili ni Jambo jema na kubwa kwa Sekta yetu ya Ujenzi, tunaamini Maboresho haya yatakwenda kurahisisha Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali, kwa Sababu Makandarasi wetu watarahisishiwa Upatikanaji wa Rasilimali Muhimu kwa Ufanisi na Utendaji Bora wa kazi ambazo wameaminiwa na Serikali kutekeleza” amesema Mhandisi Kasekenya.

Related Posts