Waziri Aweso ataka huduma ya maji safi kuimarishwa Morogoro.

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amepongeza ushirikiano baina ya Taasisi za sekta ya Maji Morogoro na kuzitaka kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha lengo la kutoa huduma ya maji ya uhakika kwa wananchi wa Morogoro linatimia.

Mhe. Aweso ameyasema hayo leo alipotembelea banda la sekta ya maji Morogoro katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki yanayoendelea katika viwanja vya NaneNane Taso, Morogoro.

Mhe. Aweso ameielekeza MORUWASA kuhakikisha kuanzia kesho wanalala saiti ili kuhakikisha malalamiko ya maji kwa maeneo ya Lukobe, Mkundi, Mindu na Mkambarani yanapata huduma ya majisafi na salama.

“maelekezo ambayo nimeyatoa kwa menejimenti ya MORUWASA lakini pia na Bodi ya MORUWASA kupitia Mkurugenzi wa MORUWASA Injinia Tamim kuanzia kesho na kuendelea ,watalala wataamka maeneo hayo ambayo nimeyataja kuhakikisha wanaongeza nguvu maeneo hayo waweze kupata huduma ya majisafi na salama” amesema Mhe. Aweso.

Related Posts