Ngao ya jamii 2024, huku moto kule balaa

COASTAL Union itakuwa timu mwenyeji kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni.

Timu hiyo iliyo chini ya kocha David Ouma inatarajia kushuka kwenye dimba hilo ikiwa na kumbukum-bu mbaya ya kupata kichapo cha mabao 3-0 kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jijini Tanga.

Rekodi zinaonyesha kwamba, tangu mwaka 2001 ambapo zilianza kuchezwa mechi za Ngao ya Jamii, Simba inaongoza kubeba taji hilo mara nyingi ambazo ni 10, inafuatia na Yanga ikichukua mara saba, kisha Mtibwa Sugar na Azam zilizochukua mara moja. Mbali na hapo, hakuna timu nyingine iliyowahi kushinda Ngao ya Jamii.

Kati ya timu nne zinazoshiriki Ngao ya Jamii mwaka huu, Coastal inaonekana ndiyo timu isiyopewa nafasi kubwa zaidi kutokana na kwamba inashiriki mara ya kwanza.

Hiyo ni kama ilivyokuwa mwaka jana ilipocheza na Singida Fountain Gate na kupoteza mechi zote mbi-li, nusu fainali na ile ya kusaka mshindi wa tatu iliyobebwa na Azam.

Licha ya Coastal kuonekana timu ngeni kwenye mchezo huo imeonyesha ushindani mkubwa Ligi Kuu Bara msimu ulioisha na kufanikiwa kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo kitendo kilichoipa nafasi ya kucheza michuano hiyo.

Rekodi kwa mechi 23 za Ligi zilizozikutanisha timu hiyo zinaibeba Azam FC ambayo imekuwa ikipata matokeo mazuri mbele ya Wagosi wa Kaya.

Zikimalizika mechi za nusu fainali, Agosti 11 ni kusaka mshindi wa tatu sambamba na fainali ya kutafu-ta bingwa ambaye atakabidhiwa taji linaloshikiliwa na Simba.

Mabingwa watetezi Simba walitwaa taji hilo baada ya kuitandika Yanga kwa penati 3-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Wakati Coastal wenyeji wa nusu fainali ya dhidi ya Azam FC wakishiriki kwa mara ya kwanza Azam FC wao ni mara yao ya sita tangu ilipopanda 2008 imeshinda mara moja mbele ya Yanga msimu wa 2016.

Kabla ya kubeba taji hilo tayari ilishacheza mara nne mfululizo na kupoteza zote kisha kwa mara ya ta-no ilishinda kibabe, mwaka huu inaingia kupambana na Coastal Union ikisaka ngao ya pili.

Coastal Union iliyomaliza msimu ulioisha Ligi Kuu Bara katika nafasi ya nne, ni kati ya timu nne zitakazoiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa msimu wa 2024/25 ikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na Simba.

Licha ya ugeni wake kwa kucheza ngao kwa mara ya kwanza watatumia mchezo huo kujiweka tayari kwaajili ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Mwanaspoti linakuletea makala katika data kati ya Coastal Union na Azam FC tkwenye mechi za Ligi Kuu Bara tangu mchezo wa kwanza hadi wa msimu ulioisha na timu hiyo kila moja kumaliza nne bora.

23-Ni idadi ya mechi zilizowakutanisha Coastal Union na Azam FC kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara tangu Septemba 2011.

13-Ni ushindi wa Azam FC kati ya mechi 23 walizokutana dhidi ya Coastal Union, matajiri wa jiji la Dar es Sa-laam ndio wababe kwani wameshinda mechi 13.

4-Ni idadi ya ushindi wa Coastal Union kwenye mechi dhidi ya Azam FC tangu wameanza kukutana 2011 hadi msimu uliomalizika.

6-Ni idadi ya sare zilizopatikana kwenye mechi za timu hizo ambapo kati ya hizo tano kati yake walifungana bao moja moja na moja walitoka suluhu.

37-Ni idadi ya mabao waliyofunga Azam FC walipokutana na Coastal, huku  Wagosi wametupia mabao 14 pekee katika mechi hizo dhidi ya Azam.

Related Posts