Shangwe ilivyo Mkoani Kigoma kwa mashabiki wa soka Mashujaa FC

Hivi ndivyo hali inayoendelea Mkoani Kigoma kwa Mashabiki wa soka Mashujaa FC wakiendelea na hamasa ambapo wametangaza tarehe 10 August 2024 kuwa kilele cha wiki ya Mashujaa Day kuelekea msimu ujao.

Ni utamaduni wa vilabu kadhaa Tanzania bara kuwa na matamasha maalumu ambayo hutumiwa kutambulisha wachezaji wapya na kuhitimishwa kwa kucheza mchezo wa kirafiki ambapo kwa Mashujaa FC watacheza na timu kutoka nchi ya Burundi.

Utambulisho wa kikosi cha Mashujaa FC kuelekea msimu wa 2024/2025 utaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Mkoa wa Kigoma na hatimaye mchezo wa kirafiki ambao utawafanya mashabiki wa Mashujaa FC kushuhudia kiwango cha kusakata kabumbu kutoka kwa kikosi kipya katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

Kwa mujibu wa takwimu zilizowahi kutolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Timu ya Mashujaa FC, yenye maskani yake mjini Kigoma, ilishika nafasi ya tatu kwa kuingiza mashabiki,Maahujaa ikiingiza mashabiki 45,638, huku Tabora United ikiwa nafasi ya nne, ikikusanya 43,808 na Azam FC, imekuwa ya tano ikiingiza jumla ya mashabiki 35,379.

 

 

Related Posts