TTCL yagusa Mahitaji muhimu ya wakulima wa Vyama vya Ushirika

Meneja wa Biashara Mkoa wa Dodoma wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Leila Pongwe akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Banda la TTCL kuhusiana huduma kwa wakulima kupata malipo ya mkupuo kwa T-PESA , kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Mwananchi akisajili namba ya laini ya TTCL kwa alama ya kidole wakati alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
*Ni katika kupata huduma ya malipo ya ya fedha kwa mkupuo
SHIRIKA la mawasiliano nchini (TTCL) limesema kuwa limejipanga kutatua changamoto za wakulima waliojiunga katika vyama vya ushirika kunufaika limewataka wakulima nchini kujiunga na vyama vya ushirika ili kunufaika na huduma ya malipo ya mkupuo inayotolewa na shirika hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Shirika hilo kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma Meneja wa Biashara Mkoa wa Dodoma Leila Pongwe amesema katika maonesho hayo wamewaletea wakulima huduma katika kuwasaidia kupokea malipo yao kwa haraka na uhakika.
“Shirika limewaletea huduma ya malipo kwa mkupuo ambayo yanamuwezesha mkulima kupitia vyama vyao vya ushirika kwa mnunuzi analipa kwa mkupuo kwa vyama na vyama vinawalipa wakulima kwa kupitia laini zao za T Pesa”,Amesema
Amesema kwa kufanya hivyo kutamsaidia mkulima kupata masoko makubwa na kufanyabiashara kwa uaminifu kwani sasa TTCL ina mkongo wa Taifa hadi nje ya nchi hivyo ni rahisi kupata huduma ya T Pesa.
Ameongeza kuwa mpaka sasa wameshaingia mikataba na vyama vya ushirika zaidi ya 100 na vyama hivyo vinapatikana kila Mkoa nchini.
Aliongeza kuwa katika maonesho hayo pia wametoa huduma ya intaneti ya bure kwa wanaotembelea maonesho hayo kunufaika na Shirika la Serikali yao.
Aidha kauli mbiu ya huduma hiyo inasema’Lipa malipo ya wakulima kwa mkupuo ukiwa na T PESA’.

Related Posts