Waandamanaji wasubiri kuundwa serikali ya mpito Bangladesh – DW – 07.08.2024

Jioni ya Jumanne, Rais wa Bangladesh alimteua Yunus, ambaye alipendekezwa na viongozi wa wanafunzi waandamanaji kama mkuu wa serikali ya mpito na kusema washiriki wengine muhimu waliosalia wanapaswa kukamilishwa hivi karibuni kuondokana na mgogoro uliopo ili kuanza mchakato kuelekea uchaguzi wa taifa hilo.

Serikali ya mpito itaziba ombwe la uongozi lililopo baada ya Mkuu wa jeshi la Bangladesh Jumatatu kutangaza kujiuzulu kwa Hasina katika hotuba yake ya kupitia televisheni iliyotolewa baada ya majuma kadhaa ya vurugu ambazo zimesababisha watu wapatao 300 kupoteza maisha na wengine maelfu kujeruhiwa.

Muhammad Yunus hajaonesha nia ya kuwania urais wa Bangladesh

Bangladesh | Machafuko huko Dhaka
Wanajeshi wa Bangladesh wakiwa katika ulinzi wakati wa amri ya kutotoka nje katika eneo la Shahbag huko Dhaka Agosti 5, 2024.Picha: Munir Uz Zaman/AFP/Getty Images

Yunus mwenye umri wa miaka 84 amenukuliwa na jarida moja akisema “Jambo muhimu ni kureja haraka kwa serikali.” Na kuongoza hana uhitaji wa kusaka kuchaguliwa au nafasi nyingine yoyote ya uteuzi baada ya kipindi cha mpito.

Amesema wanahitaji utulivu, wanahitaji mpango kuelekeauchaguzi mpya na wanahitaji kufanya kazi ili kujiandaa kwa uongozi mpya. Amesema katika  siku zijazo, atazungumza na wadau wote muhimu kutoka katika vyama vya siasa vya Bangladesh kwa kujikita katika kutafuta jinsi wanavyoweza kufanya kazi pamoja ili kuijenga upya Bangladesh na jinsi gani wanaweza kusaidia.

Na msemaji wake amesema kiongozi huyo anatarajiwa kurejea Dhaka Alhamisi baada ya kukamilisha utaratibu wa matibabu huko Paris, Ufaransa.

Jumuiya ya kimataifa yatoa himizo la amani na utulivu

Nje ya taifa hilo viongozi wengine akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameitaka Bangladesh kuheshimu demokrasia, utawala wa sheria na matakwa ya watu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong, ambae alikutana na Blinken hivi karibuni alitembelea Bangladesh amezitaka pande zote kujitenga na vurugu. Lakini kwa upande wake Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imewataka raia wake kujizuia kusafari kwenda Bangladesh kwa usalama wao.

Kujiuzulu kwa Hasina kulizusha shangwe katika maeneo tofauti ya taifa hilo ambapo umati wa watu uliingia katika makazi yake rasmi muda mfupi baada ya kutoroka taifa hilo lenye jumla ya watu milioni 170 ambalo katika miaka ya hivi karibuni limekuwa katika misukosuko ya kiuchumi.

Soma zaidi:Serikali ya mpito Bangladesh kushirikisha makundi yote

Hali ya kawaida polepole ilianza kurejea baada ya machafuko ya Jumatatu, lakini maandamano mapya yalizuka katika vitongoji vya jiji la Dhaka siku ya Jumatano wakati mamia ya maafisa kutoka benki kuu kuwalazimish manaibu magava wao wanne kujiuzulu kwa madai ya ufisadi.

Related Posts