WAFANYAKAZI TANROADS WAFANYA USAFI HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA

WAFANYAKAZI wa Wakala  ya Barabara Tanzania(TANROADS),wakifanya zoezi la usafi katika  Hospitali ya Rufaa ya Dodoma  ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

 

Fundi Sanifu Mwandamizi wa TANROADS Makao Makuu,Bw.Clement Ndagiwe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi katika barabara zinazozunguka Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na viunga vyake ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini hapa.

Afisa Habari wa Hospital hiyo, Bi. Tumaini ameishukuru TANROADS kwa kuungana nao katika kufanya usafi wa mazingira ya hospital hiyo.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAKALA ya Barabara Tanzania(TANROADS), imesema pamoja na majukumu iliyopewa kisheria pia wanalo jukumu la kuhakikisha wanashiriki katika suala zima la utunzaji wa mazingira.

Hayo yalielezwa na Fundi Sanifu Mwandamizi wa TANROADS Makao Makuu,Bw. Clement Ndagiwe,wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi katika barabara zinazozunguka Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na viunga vyake ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini hapa.

“Majukumu yetu ni pamoja na kusanifu, kujenga, kutunza na kukarabati miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na madaraja, lakini pia tunapaswa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira,” alisema Bw. Ndagiwe.

Pia Bw. Ndagiwe alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kuendelea na tabia ya kutunza mazingira ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza kutokana na kutupa takataka hovyo

Alisema wameamua kuchagua kufanya usafi katika eneo la hospitali kwa kuwa hapo kuna wagonjwa hivyo ni sehemu ya kijamii ambayo inapaswa kuwa safi muda wote na hata wagonjwa wanapoona hivyo wanapata faraja wakiamini kuna watu wanawakumbuka na kuwathamini.

“Pia huu ni muendelezo wa shughuli mbalimbali tulizofanya ikiwa ni sehemu ya ushiriki wetu kwenye maonesho ya Nanenane Kitaifa, na tunabanda wataalam wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu mambo mbalimbali tunayoyafanya,” amesema Bw. Ndagiwe.

Kwa upande wake Afisa Habari wa Hospital hiyo, Bi. Tumaini ameishukuru TANROADS kwa kuungana nao katika kufanya usafi wa mazingira ya hospital hiyo.

Naye mkazi wa Ihumwa, amesema taasisi nyingine ziige mfano wa TANROADS katika kujumuika na jamii katika utunzaji wa mazingira.

Related Posts