NIGERIA imewashikilia baadhi ya mafundi cherehani kwa kutengeneza bendera za Urusi ambazo zilipeperushwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali wiki hii katika majimbo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).
Idara ya Huduma za Serikali ya Nigeria (DSS) pia ilisema kwenye chapisho kwenye mtandao wa X kwamba imewaweka kizuizini baadhi ya wafadhili wa mafundi cherehani bila kufafanua.
Imesema uchunguzi unaendelea. Haikusema ni mafundi cherehani au wafadhili wangapi walikuwa wamezuiliwa.
Katika majimbo ya kaskazini ya Borno, Kaduna, Kano na Katsina, waandamanaji walionekana wakipeperusha mamia ya bendera za Urusi huku wengine wakitaka kutwaliwa kwa jeshi.
Mkuu wa Majeshi nchini humo, Jeneral Christopher Musa amewaeleza waandishi wa habari kuwa; “Tumewatambua wanaowafadhili na tutachukua hatua kali dhidi ya hilo.”
Mamia ya maelfu ya Wanigeria wamekuwa wakiandamana tangu tarehe 1 Agosti mwaka huu dhidi ya mageuzi maumivu ya kiuchumi ya Rais Tinubu ambayo yamesababisha kuondolewa kwa sehemu ya ruzuku ya petroli na umeme, kushuka kwa thamani ya sarafu na mfumuko wa bei ambao umevunja rekodi ya miongo mitatu