Haya hapa yanayomsubiri Kylian Mbappe Hispania

MADRID HISPANIA: LA Liga inatarajiwa kuanza Agosti, huku mashabiki wa soka duniani wakisubiri kuona kile ambacho mastaa wapya waliosajiliwa na timu mbalimbali za ligi hiyo watakachofanya.

Mmoja kati ya wachezaji ambao wanasubiriwa kwa hamu ni Kylian Mbappe ambaye amejiunga na Real Madrid kwa usajili huru baada ya kumaliza mkataba wake na PSG.

Wakati mashabiki wakimsubiri Mbappe, rekodi nazo zinamsubiri staa huyo aliyewahi kuhusishwa na wababe hao wa Hispania kwa muda mrefu kabla ya kutua dirisha hili.

Hapa tumekuletea rekodi mbalimbali ambazo staa huyu atatakiwa kuzivunja ndani ya Madrid na La Liga kwa jumla.

Kimsingi Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji aliyewahi kuchukua tuzo nyingi (5) zaidi za Ballon d’Or katika historia ya klabu hiyo ambazo alishinda nne akiwa na timu hiyo na moja akiwa na Manchester United.

Mbappe mwenye umri wa miaka 25, ambaye amewahi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hizo mara sita, moja ya kazi kubwa inayomsubiri Madrid ni kuivuka rekodi hii ya Ronaldo.

Mfungaji bora wa muda wote Madrid

Hadi anaondoka Ronaldo alikuwa amecheza mechi 438 za kiushindani na kufunga mabao 450, akiwa ndio mchezaji aliyefunga mara nyingi zaidi katika historia ya timu hiyo.

Mbappe ambaye akiwa na PSG amefunga mabao 256 katika mechi 308 akiwa pia ndiye mfungaji bora wa muda wote wa matajiri hao, moja ya rekodi zinazomsubiri kuzivunja ni hiyo ya utupiaji ya Ronaldo.

Mbali ya rekodi hiyo ambayo itahitaji zaidi ya msimu mmoja kuifikia, kuna rekodi ya kufunga mabao 50 katika mechi chache katika La Liga inayoshikiliwa na Isidro Langara aliyefikisha katika mechi 37.

Mbai ya rrekodi za Ronaldo Mbappe anatakiwa kuvunja rekodi ya Mfaransa mwenzake Karim Benzema kwa kutoa pasi nyingi za mabao ndani ya timu hiyo.

Benzema anashikilia rekodi hiyo kwa pasi zake 165 akiwa ndio kinara.

Kutupia sana Ligi ya Mabingwa

Licha ya kuwa na umri mdogo, Mbappe tayari ni mmoja wa washambuliaji mahiri wa Ligi ya Mabingwa.

Mfaransa huyo ana mabao 48 kwenye michuano hiyo akiwazidi mastaa kibao kama  Neymar, Eusebio, Mohamed Salah, Didier Drogba, Samuel Etoo, Alessandro Del Piero, Romario, Sergio Aguero, Ferenc Puskas, Gerd Muller, Wayne. Rooney, Luis Suarez, na David Trezeguet.

Vile vile yupo katika orodha ya wachezaji 10 waliofunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiungana na mastaa kama Robert Lewandowski, Alfredo di Stefano, Ruud van Nistelrooy, Lionel Messi na Cristiano.

Vilevile Mbappe ndiye mfungaji mabao mdogo zaidi wa Ligi ya Mabingwa kwa timu mbili, akiwa ndio kinara pale  PSG huku Monaco akishika nafasi yapili.

Kwa sasa, Ronaldo mwenye mabao 107 ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi akiwa na Madrid katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Mbappe inamsubiri rekodi hii.

Lionel Messi ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye El Clasico, akiwa amefunga mabao 26 dhidi ya Real Madrid.

Lakini Mbappe anaweza kuifikia na kuivuka rekodi hiyo kwani tayari ana mabao sita dhidi ya Barca katika mechi nne pekee alizocheza nao akiwa PSG.

Pia staa huyu ni mmoja kati ya wachezaji watatu waliofunga hat trick ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barca.

Vilevile ndio mchezaji wa kwanza kuifunga Barca mabao manne katika shindano moja la Ligi ya Mabingwa, hivyo anaonekana kuwa huenda akaifikia rekodi ya Messi ikiwa ataendelea kufanya alichokuwa anakifanya.

Messi ndio anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi katika msimu mmoja wa La Liga pale alipofanya hivyo msimu wa 2011/12 alipoweka kambani mabao 50.

Mbappe hii pia inamsubiri.

Related Posts