Mshukiwa wa njama ya mauaji kwenye tamasha la Taylor Swift ‘alipanga kuua watu wengi iwezekanavyo’

Polisi nchini Austria wamewahoji vijana watatu wanaoshukiwa kupanga shambulizi la kujitoa mhanga katika onyesho la Taylor Swift wikiendi hii.

Mashirika ya kijasusi ya kigeni yalisaidia mamlaka kufichua mpango huo unaodaiwa, kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Gerhard Karner.

Chanzo kinachofahamika kiliiambia CNN kwamba Marekani ilitoa onyo kwa mamlaka mjini Vienna.

Waandalizi walighairi matamasha matatu, ambayo yalipangwa kufanyika katika mji mkuu wa Ulaya kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi. CNN imewasiliana na wawakilishi wa Swift kwa maoni.

Wachunguzi waligundua  kemikali, vifaa vya vilipuzi, vilipuzi na euro 21,000  pesa ghushi nyumbani kwa mshukiwa mkuu,wa ISIS mwenye umri wa miaka 19  kulingana na mamlaka.

Kijana huyo – ambaye alikamatwa Jumatano asubuhi katika mji wa mashariki wa Ternitz  alipanga kujiua mwenyewe na “idadi kubwa ya watu,” kulingana na mkuu wa shirika la kijasusi la ndani, Omar Haijawi-Pirchner.

“Alisema alikusudia kufanya shambulizi kwa kutumia vilipuzi na visu,” Haijawi-Pirchner aliwaambia waandishi wa habari mjini Vienna siku ya Alhamisi. “Lengo lake lilikuwa kujiua mwenyewe na idadi kubwa ya watu wakati wa tamasha, leo au kesho.”

Washukiwa wengine wawili walizuiliwa, wenye umri wa miaka 17 na 15.

Mvulana huyo wa miaka 17 alifanya kazi katika kampuni ya vifaa ambayo ingetoa huduma katika eneo la tamasha.

Related Posts