Mutale: Mambo matamu yanakuja | Mwanaspoti

WINGA wa Simba, Joshua Mutale amesema kicheko kwa mashabiki wa timu hiyo ni suala la muda, akiwapa ahadi yanayokuja mbele yao yanafurahisha, kwani wamejipanga kufanya makubwa msimu ujao.

Mutale aliyesajiliwa na timu hiyo, akitokea Power Dynamos ya Zambia, alisema anafahamu mashabiki wameumia kufungwa na Yanga bao 1-0 nusu fainali ya Ngao ya Jamii, lakini amewaomba kuyasahau na kuelekeza nguvu katika majukumu mbalimbali yaliopo mbele yao.

“Hatuna budi kupambana ndio kwanza tunakwenda kuyaanza majukumu mazito mbele yetu, mashabiki tushikamane kwa pamoja kwenda kuyatimiza yale wana

“Mashabiki wasichoke, tuungane kwa pamoja kuyapambania malengo yetu ya msimu ujao, mchezo dhidi ya Yanga tumecheza vizuri ingawa upande wa matokeo haikuwa bahati yetu.

Aliongeza”Ni imani yangu tutakuwa na msimu mzuri ambao utawapa furaha mashabiki, kubwa zaidi malengo ya kwanza ni ubingwa katika mashindano ambayo yatakuwa mbele yetu.”

Mbali na hilo, alikiri mabeki wa Yanga walifanya kazi ngumu ya kuzuia mashambulizi yao “Walikuwa na umakini, kutokana na mashambulizi ambayo tulikuwa tunawapelekea, ila naamini tukiendelea kuzoeana, Simba hii ni hatari zaidi.”

Related Posts