BONGO Fleva inazidi kuchacha mbuga.Sio kwenye soko la ndani tu,m hadi kimataifa na tofauti ya miaka ya nyuma ilikuwa wimbo kutoka nje ya mipaka ya nchi, huwa ni jambo la kushangaza na litazungumzwa kila siku.
Hata hivyo, miaka ya karibuni imekuwa ni kawaida na wasanii wa Bongo Fleva wameliteka soko la muziki duniani na kuanzia nyimbo zao kutesa kwenye chati kubwa hadi kufanya shoo kubwa sio stori kubwa tena.
Ni juzi tu, wimbo ‘Comment Ca Va’ au Komasava kama tunavyoutamka kiswahili aliofanya ‘remix’ na mkali kutoka Marekani, Jason Derulo na Chley Nkosi na Khalil Harrison kutoka Afrika Kusini sasa uko kwenye chati za Billboard. Ni hatua kubwa sana muziki wa Bongo Fleva umepiga.
Mbali na kukua kwa kasi, hata hivyo, wapo wasanii ambao ukuaji wao kisanii hulazimisha kwa maana ya kutumia njia za kujitangaza hata kama si wakali wa mashairi.
Ni kama wanalazimisha kuwafikia mashabiki wa muziki kwa kutafuta ‘kiki’ yaani kufanya matukio yanayosababisha watu wawafuatilia na kisha wanaachia ngoma na ndipo mashabiki wanajua aliyeimba ni nani.
Hata hivyo, wapo wale ambao kiki kwao sio ishu, kazi zao tu ni kiki tosha na mashabiki ni kama wanakuwa wanazisubiri kazi zao kwa hamu kutokana na uwezo wao na wala hawatumii nguvu nyingi kusukuma kazi zao kukubalika kwa mashabiki.
Ni mmoja wa wasanii wakongwe kwenye Bongo Fleva na amekuwa kipenzi cha mashabiki wa muziki huo kwa muda mrefu.
Ukongwe wake kwenye burudani ndio umesababisha kujitanua zaidi na sasa anamiliki kituo cha redio cha Crown FM na Crown Media ili kuendelea kutanua wigo wa muziki wa Bongo Fleva kwake na wasanii wengine.
Sifa kubwa ya Kiba, ni mashairi yake kupenya kwa kasi kwenye mioyo ya mashabiki na kujikuta hatumii nguvu kubwa kusukuma kazi zake na hii ni kutokana na uwezo wa kutunga na sauti yake. Hahitaji kiki.
Kipaji ngeni kwenye Bongo Fleva lakini kimeshateka hisia za mashabiki wengi. Sauti yake ya kipekee imemfanya awe mmoja wa wasanii wanaovutia kumsikiliza kila anapoachia wimbo.
Tangu alipotoka kimuziki mwaka 2022 na wimbo wake wa kwanza ‘Mbwembwe’ ulimwingizia watazamaji zaidi ya 11,000 na wamekuwa wakiongezeka kila anapoachia video na ngoma zake.
Mwaka jana alitoa wimbo wa ‘Watu Feki’ ambao ndani yake ameeleza ubaya wa marafiki na kupokewa na mashabiki wake bila hata ya kuusukuma kwa kiki tofauti na wasanii wengi wanaopenda kufanya hivyo.
Umepita mwaka mmoja tangu aachie kibao hicho ambacho hadi sasa kinafanya vizuri na kimeingiza watazamaji Milioni 2 kwa video na Milioni 1 kwa upande wa audio.
Kwa sasa anatamba na albamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Therapy’ iliyotoka miezi mitatu iliyopita yenye ngoma 14 ambazo ndani yake amewashirikisha baadhi ya wasanii.
Msanii huyo ambaye ni mtunzi wa nyimbo za mapenzi amekuwa na kismati kila anapotoa wimbo wake unakuwa na mapokezi mazuri kwa mashabiki zake.
Wimbo kama ‘Nakupenda’, ‘Sugar’, ‘Sawa’ na ‘Nitasema’ ni miongoni mwa ngoma zilizofanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii hasa Youtube ikiingiza zaidi ya watazamaji Milioni 10.
Mapokezi makubwa ya ngoma zake yanaanzia Tiktok na akitoa kionjo cha ngoma yake tu kinakuwa na mapokezi makubwa hata kabla ya wimbo kutoka.
Ni miongoni mwa zao lililotokea kwenye akademi ya kukuzia vipaji (THT) walikopita wasanii mbalimbali kama Linah, Nandy, Ruby, Jay Melody na wengine.
Ni msanii ambaye yuko bize na kufanya kazi zake zaidi kuliko kiki na ngoma ya Iokote aliyomshirikisha Hanstone ni miongoni mwa ngoma zilizomuingizia mkwanja mrefu.
Mbali na kutofanya kiki lakini ni mmoja wa wasanii wa kike ambaye hawapendi kuweka wazi sana ishu zake binafsi kama mahusiano na familia yake.
Mkali wa kibao cha ‘Hakuna Matata’ ambao umewavutia wengi akiwemo Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ambaye tangu Marioo katoa wimbo huo amekuwa akiucheza.
Kwa sasa anafamika kwa kutoa ngoma za Amapiano ambayo asili yake ni kutoka Afrika Kusini, nyimbo kama ‘Tomorrow’, ‘Dear EX’, ‘Beer Tamu’ na ‘Mama Amina’ zilizofanya vizuri.
Rapa huyo ambaye pia ni mume wa msanii wa kizazi kipya, Nandy, imekuwa ikiongea zaidi mistari yake kuliko kufanya kiki za mitandaoni kupromoti ngoma.
Hadi sasa kuna ngoma kama ‘Puuh’ aliomshirikisha Jay Melody, ‘Maokoto’ alioimba na Marioo ni ngoma zilizofanya vizuri kwenye mitandao yake ya kijamaii.
Mara chache sana kumuona akifanya shoo na inawezekana ndani ya mwaka mzima akitumbuiza jukwaani zaidi ya kutoa ngoma.
Mkongwe huyo wa muziki wa Hip hop ni ngumu mara nyingi anapotoa ngoma zinaenda mjini zenyewe bila ya kutumia propaganda nyingine.