TBL yashiriki maonyesho ya Nanenane kuwaunga mkono wakulima

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

Kampuni ya bia TBL imejumuika na Watanzania kote nchini kuadhimisha Siku ya Wakulima, ambayo inaadhimishwa kitaifa mkoani Dodoma. Hafla hii inatoa fursa ya kuonyesha mshikamano wa kampuni na wakulima ambao ni sehemu muhimu katika uzalishaji wa malighafi zinazotumika kutengeneza vinywaji vyenye mvinyo.

Huu ni mwendelezo wa jitihada mbalimbali ambazo TBL imekuwa ikizifanya kwa wakulima wa shayiri, mtama na zabibu, mazao haya yakiwa ni muhimu katika utengenezaji wa bia. Kampuni ya TBL na TDL imedhamiria kuboresha maisha ya wakulima wadogo kwa njia mbalimbali, ikiwemo kutoa mafunzo, mbinu za kilimo, pamoja na pembejeo za kilimo. Hatua hizi zimekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya shayiri na mtama  hapa nchini.

Akizungumza katika mabanda ya TBL mkoani Dodoma, Bwana. Jacob Mwavika Afisa Kilimo kutoka TBL alisema, “Kwa muda mrefu, tumekuwa tukichukua hatua mbalimbali za kuwasaidia wakulima wadogo hapa nchini. Tumeweza kutoa mafunzo ya kitaalamu, vifaa vya kilimo, na pembejeo muhimu kwa wakulima. Aidha, tumefanikiwa kuingia mikataba na wakulima wengi ambao mazao yao yanatumika katika utengenezaji wa bia katika kiwanda chetu.”

Bwana Jacob alisisitiza kuwa uwekezaji wa TBL katika wakulima wa ndani umekuwa na faida kubwa, Kupitia kilmo cha mkataba na wakulima, TBL inaendeleza lengo la kuboresha uzalishaji wa ndani na kukuza uchumi wa taifa.

Katika hatua nyingine, TBL imeandaa mipango ya kuendelea kua karibu na kuimarisha uhusiano na wakulima kwa kuongeza ushirikiano katika nyanja za kilimo. Kampuni pia inamikakati kuendeleza miradi ya maendeleo ya kilimo ambayo itaendelea kuboresha hali ya maisha ya wakulima na kuongeza tija katika sekta ya kilimo.

Kampuni ya TBL ina imani kubwa kwamba jitihada hizi zitachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa sekta ya kilimo nchini, na kuleta maendeleo endelevu katika jamii za wakulima.

Related Posts