Washitakiwa 9 wa mauaji ya mtoto Asimwe wafikishwa tena mahakamani

Ni muendelezo wa ripoti ya kesi ya washitakiwa tisa wa mauaji ya mtoto Asimwe Novart aliyekuwa na ualbino ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu may 30,2024 na June 17,2024 mwili wake ulikutwa kwenye kalavati akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake

Washitakiwa hao tisa leo August 8 wamefikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba kwa ajili ya kutajwa tena shtaka lao

Wakili wa serikali Erick Mabagala amesema kuwa bado wanaendelea na mchakato wa kukamilisha mwenendo kabidhi yaani (commital) kwa ajili ya kupeleka kesi hiyo mahakama kuu ambayo ndo ina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia na uchunguzi wa shauri hilo no 17740 la mwaka 2024 tayari umekamilika

Katika shauri hilo mshitakiwa namba tatu Nurdin Ahmada ameiomba mahakama hiyo kuandika maelezo ya awali japo hakukubaliwa baada ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba Elipokea Yona Wilson kusema kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo ataweza kutoa maelezo yake wakati wa utetezi pindi kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa

Watuhumiwa hao tisa ni Elpidius Alfred Rwegoshora miaka 49 ambaye ni padri,Novat Venant miaka 24 ambaye ni baba wa mtoto Asimwe,Nurdin Ahmada,Ramadhan Selestine,Rwenyagira Alphonce,Dastan Buchard, Faswiu Athuman,Gozibert Arikad na Dezdery Everigist

Watuhumiwa hao tisa hawakuruhusiwa kujibu chochote na wamerudishwa rumande mpaka August 23 kesi yao itakapoitwa tena kwa ajili ya kutajwa

Related Posts