KILELE CHA MAONESHO NANENANE LINDI, DC RUANGWA ATEMBELEA BANDA LA TBS

MKUU wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma ametembela banda la ShIrika la Viwango Tanzania (TBS) katika siku ya kilele cha Maonesho ya Nanenane ambayo yamefanyika katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

DC Ngoma amefika katika banda hilo na kujionea maafisa wa TBS wakotoa elimu na kuwahudumia wananchi ambao wametembelea banda lao.

DC Ngoma ameelezwa namna TBS inavyofanya shughuli zake katika kuhakikisha wazalishaji, wauzaji na wasambazaji wa bidhaa pamoja na wananchi kwa ujumla wanatumia bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya viwango.






Related Posts