Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akutana na kuzungumza na Viongozi Makampuni ya Uwakala wa Meli ya Nyota Tanzania LTD (MAERSK Tanzania) na Sturrock Flex Shipping LTD jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yake ametumia fursa hiyo kuwaeleza kuhusu maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali katika Miundombinu ya Bandari ikiwemo Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na Bandari za Maziwa nchini, Ukarabati na Ujenzi wa Meli, Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR na maboresho katıka reli ya Kati na kuwasisitiza kutumia fursa hiyo kwa kuendelea kushawishi mashirika Mengi zaidi kutumia Bandari ya Dar es Salaam na Bandari nyingine zilizopo nchini.
Aidha, Naibu Waziri Kihenzile amewaahidi kufanyia kazı changamoto zote zilizowasilishwa ili kutokwamisha shughuli za uchukuzi nchini.