BENKI YA MWANGA YAFANYA MKUTANO MKUU WA NNE WA MWAKA KWA WANAHISA WAKE MKOANI KILIMANJARO

Mwenyekiti  wa Bodi ya  Wakurugenzi ya Mwanga Hakika Benki, Mhandisi Rithuan Mringo (watatu kushoto), akizungumza na wanahisa wa benki hiyo wakati wa Hafla ya Mkutano Mkuu wa nne wa wanahisa wa Benki hiyo uliyofanyika Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Jagjit Singh, Makamo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mwanga Hakika benki  Mhandisi Raymond Thadeus , Pamoja na viongozi wengine wa bodi hiyo.

Makamo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mwanga Hakika benki  Mhandisi Raymond Thadeus (wapili kushoto), akizungumza na wanahisa wa benki hiyo wakati wa Hafla ya Mkutano Mkuu wa nne wa wanahisa wa Benki hiyo uliyofanyika Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Jagjit Singh, Mwenyekiti  wa Bodi ya  Wakurugenzi ya Mwanga Hakika Benki, Mhandisi Rithuan Mringo Pamoja na viongozi wengine wa bodi hiyo.

Wanahisa wa Mwanga Hakika Bank wakiwa katika usahili kwaajili ya kushiriki Mkutano huo.

Wanahisa wa Mwanga Hakika Bank wakifuatilia Mkutano huo.

Benki ya Mwanga Hakika Imefanya mkutano mkuu wa nne na wanahisa wa benki hiyo yaani AGM (Annual General Meeting) wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Mkutano huu una lengo la kutimiza matakwa ya serikali inavyoagiza kila kampuni kufanya mkutano mkuu na wanahisa wao kila mwaka.

Akizungumza wakati ,mkutano huo  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi  wa Mwanga Hakika Benki Mhandisi Ruthuan Mringo ameeleza kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri  yaliyopo baina ya wanahisa na benki yao, ili kuwataarifu wanahisa  kuhusu benki ilipoanza ilipo sasa na mwendelezo wake ili kuweza kupata taarifa kamili na Ili wanahisa hao waweze kutathmini maendeleo ya benki hiyo na kubaini kama Kuna changamoto ziweze kutatuliwa. 

 Pia wanahisa  wanayo nafasi kubwa ya kutoa ushauri juu ya maswala ya kimaendeleo yatakayo ikuza benki hiyo ili iendelee kuwa imaara siku hadi siku.

Mkutano huu ni mkutano wa nne na wanahisa wa benki ya Mwanga Hakika, ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka  (2021) na kuhudhuriwa na wanahisa mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wao na wanahisa wa benki hiyo. Amesema Mringo.

Mbali na hayo, benki ya Mwanga Hakika imekuwa ni desturi yetu kufanya mkutano huo wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro kwasababu benki hiyo ch

Benki hiyo imeendelea kuimarika siku hadi siku na kwamba tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020 kumekuwepo ongezeko la amana za wateja kutoka Sh80.06 bilioni kwa mwaka 2022 hadi kufikia Sh142.19 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 78.

Aidha amesema ukuaji wa mikopo kwa wateja umeongezeka kutoka Sh80.69 bilioni hadi kufikia Sh131.44 bilioni.

“Ukuaji huu unaonyesha uwezo wetu wa kusaidia wateja wetu kufikia malengo yao ya kifedhabkwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu,”amesema Mringo 

Amesema jumla ya mali za benki hiyo zimeongezeka na kufikia Sh208.93 bilioni, ikilinganishwa na Sh116.95 bilioni mwaka 2022 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 79.

“Mapato yetu ya Benki yamefikia Sh20.06 bilioni kutoka Sh 13 .41 bilioni mwaka 2022, ongezeko la asilimia 50 , ukuaji huu unatokana na juhudi zetu za kuboresha huduma na kuongeza Wigo kwa wateja wetu,”amesema Mringo

Related Posts