KIDO Balozi wa Kampeni ya USAID ya “Holela-Holela Itakukosti” Atinga kwenye Siku ya Nane Nane

Dkt. Salum Manyatta, Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu sehemu ya Afya Moja akiwa na KIDO wakijadili kuhusu kampeni ya “Holela Holela Itakukosti” inayolenga kupambana na Usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa (UVIDA) na magonjwa ya zuonotiki (magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Nane Nane huko Dodoma katika viwanja vya Nzuguni. Kampeni hii inaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kutekelezwa na Wizara ya Afya, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Ofisi ya Makamu Rais (Mazingira) na kufadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION. Kampeni ya “Holela-Holela Itakukosti” imeendelea kutoa elimu katika maadhimisho ya Siku ya Nane Nane kupitia KIDO, balozi wa kampeni, ambaye alivaa vazi la kidonge chenye rangi nyekundu na njano ili kuhimiza utumiaji wa mbinu sahihi za kilimo na ufugaji ili kupambana na UVIDA na magonjwa ya zuonotiki

KIDO ambaye ni Balozi wa kampeini ya Holela-Holea Itakukosti akiwa kwenye picha na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ihala mara baada ya kuwapa elimu juu ya na Usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa (UVIDA) na magonjwa ya zuonotiki (yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Nane Nane katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma. Kampeni hii inaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kutekelezwa Wizara ya Afya, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Ofisi ya Makamu Rais (Mazingira) na kufadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION. KIDO ni balozi wa kampeni hii ambaye huvaa vazi la kidonge chenye rangi nyekundu na ya njano na anaendelea kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua sahihi za kiafya na usalama ili kuzuia Usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa (UVIDA) na magonjwa ya zuonotiki.

DODOMA Agosti 10 2024 Katika maadhimisho yenye shamrashamra na ubunifu wa kilimo na uwajibikaji, KIDO—balozi wa kampeni ya “Holela-Holela Itakukosti”—amejishughulisha kikamilifu na wakulima na wafugaji wakati wa Siku ya Nane Nane mwaka huu. Kampeni ya Holal-Holela ambayo inafadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa(USAID) na kutekelezwa na mradi wa Breakthrough ACTION, kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo, na Wizara ya Afya, inalenga kukuza mbinu za kupambana na Usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa (UVIDA) na magonjwa ya zuonotiki, ikisisitiza jukumu muhimu la wakulima katika kulinda afya ya umma na kuboresha usalama wa chakula.

Katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, KIDO alishirikiana na wakulima na wafugaji wa ndani kuibua mijadala iliyoratibiwa an alishiriki katika kutoa maarifa juu ya mbinu endelevu za kilimo. Akisisitiza ujumbe wa kampeni, “uzembe ni gharama,” KIDO alionyesha jinsi kilimo chenye uwajibikaji kinavyoweza kulinda maisha na afya ya jamii.

Kampeni ya “Holela-Holela Itakukosti” inahimiza wakulima kufuata hatua za kinga dhidi ya matumizi mabaya ya dawa hasa antibiotiki katika kilimo, ikitetea mbinu zinazowajibika ambazo zinahakikisha afya ya umma. Wakati wa mijadala, KIDO aliwasihi wakulima kutafakari juu ya tabia zao na jinsi zinavyoweza kuchangia kusambaza janga la UVIDA na magonjwa ya zuonotiki. Alizungumzia masuala ya kawaida kama vile usafi duni katika ufugaji wa wanyama na matumizi ya dawa bila ushauri wa wataalam wa mifugo, akihimiza wakulima kushiriki uzoefu wao. KIDO alisisitiza mbinu madhubuti kama kunawa mikono ipasavyo, usafi katika mabanda ya wanyama, na kushauriana na wataalamu wa mifugo kabla ya kutumia dawa.

Katika maadhimisho hayo, KIDO aliongoza vipindi vya kutoa elimu juu ya magonjwa ya zuonotiki, ambayo yanaweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na kuleta tishio kubwa kwa afya ya umma. Alisisitiza kwamba wakulima ndio mstari wa mbele katika kujikinga dhidi ya magonjwa hayo kupitia mbinu rahisi na fanisi za usafi binafsi kama kunawa mikono, usafi wa mazingira hasa mabanda ya kufugia wanyama, kutumia vifaa kinga kama buti. KIDO alisisitiza umuhimu wa chanjo na kufuata miongozo ya wataalamu wa mifugo, akionyesha jinsi hatua hizi za kinga zinavyoweza kuboresha afya ya wanyama na jamii.

Dk. Salum Manyatta, Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Afya Moja, alikiri mchango wa KIDO wakati wa Siku ya Nane Nane, “Kama balozi wetu, KIDO anaonyesha uhusiano muhimu kati ya kilimo, afya ya binadamu, wanyama, na mazingira ni muhimu kwa ajili ya mustakabali endelevu. Kupitia ushirikiano wa KIDO, tunawawezesha wakulima kwa maarifa na zana zinazohitajika kupambana na UVIDA na magonjwa ya zuonotiki.”

Msisimko ulioletwa na ushirikiano wa KIDO katika Siku ya Nane Nane haukuzingatia tu hitaji la haraka la kuchukua hatua dhidi ya UVIDA na magonjwa ya zuonotiki bali pia ulitambua mchango mkubwa wakulima wa Tanzania. Kwa kujitolea na ushirikiano unaoendelea, kampeni ya “Holela Holela Itakukosti,” inayoongozwa na KIDO, inasimama kama taa ya matumaini kwa mazingira ya kilimo yenye afya na endelevu zaidi nchini Tanzania.

Related Posts