Hamas yataka utekelezaji wa mpango wa amani wa Biden Gaza – DW – 12.08.2024

Hamas imewahimiza wapatanishi wa mzozo wa Gaza kutekeleza mpango wa usitishaji vita uliowasilishwa na Rais wa Marekani Joe Biden badala ya kufanya mazungumzo zaidi, wakati Wapalestina wakikimbia operesheni mpya ya Israel.

Taarifa kutoka kundi hilo ambalo shambulio lake la Oktoba 7 lilisababisha vita vya Israel, imekuja siku moja baada ya shambulio baya zaidi dhidi ya Gaza, katika zaidi ya miezi 10 ya vita.

Soma pia:Jeshi la Israel laamuru watu kuondoka kusini mwa Gaza 

Wapatanishi wa kimataifa wamezialika Israel na Hamas kurejea kwenye mazungumzo ya usitishaji vita wa muda mrefu, na kuachiliwa kwa mateka baada ya kuuawa kwa viongozi wenye mafungamano na Iran, kuzidisha wasiwasi katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Ukanda wa Gaza Gaza | Uharibifu baada ya shambulio la Israeli shuleni
Mashambuzi ya Israel yameua watu wasiopungua 100 GazaPicha: Mahmoud Zaki/XinHua/dpa/picture alliance

Israel ambayo Waziri Mkuu wake Benjamin Netanyahu ameshtumiwa kurefusha vita hivyo kwa manufaa binafsi ya kisiasa, imekubali mwaliko kutoka Marekani, Qatar na Misri kwa mazungumzo yaliopangwa kufanyika Alhamisi wiki hii.

Soma pia:Israel yaapa kumwangamiza kiongozi mpya wa Hamas 

Hamas imesema jana inataka utekelezaji wa mpango wa mapatano ulioainishwa na Biden Mei 31, na baadae kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Related Posts