MARIOO ASHINDA KESI YA MADAI ALIYOTAKIWA KULIPA MILIONI 500 – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mahakama Kuu Arusha imeitulipia mbali Kesi iliyokuwa inamkabili msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Omary Ally Mwanga alimaarufu kama Marioo.

 

 

Katika kesi hiyo Marioo alishtakiwa yeye pamoja na meneja wake Sweetbert Charles Mwinula na Kampuni ya Kismaty Advert Media Co. Ltd, Kampuni inayojihusisha na uandaaji wa matamasha na shughuli zinazohusiana na burudani yenye makao yake jijini Arusha.

 

 

Kampuni hiyo ilimshtaki Marioo mwaka 2022 Arusha ikimdai malipo ya jumla ya Sh550 milioni, kwa kuvunja mkataba wa utumbuizaji.

 

 

Marioo ameshinda Kesi hiyo ya madai namba 29/2022 na Mahakama kuamuru kampuni hiyo kumlipa Marioo gharama za Usumbufu.

 

 

CHANZO : Bongo 5

Related Posts