Mashabiki wa soka Tanzania kusherehekea EPLna Guinness

 

BIA rasmi ya Ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2024/25, Bia ya GUINNESS kwa kutambua kuwa mpira wa miguu unahusu zaidi mashabiki, wametangaza kushirikiana na Club 1245 ya Masaki Jijini Dar Es salaam kukuletea jukwaa maalum la kujumuika pamoja kushuhudia ladha na utamu wa mechi zote za Ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2024/25.

Lengo la mashirikiano hayo ya GUINNESS na Club 1245 ni kutoa sapoti na kuikuza familia ya wapenda soka nchini Tanzania nje na ndani ya viwanja vya soka na kuhamasisha na kukuza maingiliano na mahusiano kati ya wateja wa bia ya GUINNESS pamoja na mashabiki wa soka la nchini Uingereza.

Ijumaa hii ya Agosti 16, 2024 pamoja na siku nyingine zote kwa msimu wa 2024/25, Shabiki wa soka la EPL atapata msisimko na kumbukumbu isiyosahaulika pamoja na wapenda soka wengine, kwa kushuhudia upekee na uzoefu kamili wa GUINNESS EPL kwenye runinga kubwa na za kisasa zilizofungwa kwenye kona zote za Club 1245 Masaki Jijini Dar es salaam, sehemu pekee tunapokutana wanamichezo na mashabiki wa EPL.

Ligi kuu ya Uingereza ndiyo ligi maarufu zaidi duniani na inayotoa fursa nzuri ya kuendeleza mafanikio ya Chapa ya GUINNESS duniani kote na kuungana na Jumuiya na washkaji wapenda soka ili kufurahi ladha na burudani ya soka la kibabe linalotimua vumbi nchini Uingereza.

About The Author

Related Posts