Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 12 Agosti 2024, amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Vietnam nchini, Mhe. Vu Thahn Huyen. Hafla hiyo imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, ikiashiria kuanza kwa majukumu rasmi ya balozi huyo hapa nchini.
Hatua hii inatarajiwa kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam katika sekta mbalimbali.
#KonceptTvUpdates