Serikali yatangaza ajira 224 kwenye taasisi 14

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza ajira 224 kutoka taasisi 14, zikiwemo za utafiti.

Nafasi hizo za ajira zilizotangazwa jana Agosti 11, 2024  ni kutoka Taasisi za Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (Taliri), Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (Ruwasa) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi (Nactvet).

Pia, ipo Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Uwekezaji wa Nyumba kwa Watumishi (WHI), Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico), Baraza la Sanaa la Taifa (NAC), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) na Wakala wa Huduma za Ununuzi wa Umma (GPSA).

Taasisi nyingine ni Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS).

Kwa upande wa Tafiri, nafasi zilizotangazwa ni mbili za mtafiti msaidizi wa ufugaji wa samaki, mtafiti msaidizi wa sayansi ya viumbe maji, mtafit msaidizi wa sayansi uvumbi nafasi moja kila kada.

Kada nyingine ni mtaalamu wa teknolojia maabara-nafasi tano na nafasi moja kwa mtaalamu wa mikrobiolojia, mtaalamu wa teknolojia utafiti uvuvi- nafasi moja.

Kwa upande wa tasisi ya Taliri, nafasi 14 zimetangazwa za wasaidizi wa eneo la shamba ngazi ya pili na muendesha mitambo- nafasi tatu.

Idara ya maji Ruwasa, nafasi za ajira ni mhandisi wa barabara- nafasi 30, mhandisi wa maji- nafasi nafasi 65.

Kwa Taasisi ya Elimu Tanzania, mchoraji picha -nafasi mbili, mtaalamu wa uchapaji- nafasi nne pamoja na mtaalamu wa maendeleo ya mitaala- nafasi moja.

Taasisi ya Nactvet, nafasi zilizotangazwa ni nafasi moja ya mtaalamu wa Tehama (ICT), mtaalamu wa uandikishaji nafasi mbili, ofisa ubora -nafasi nne.

Kwa upande wa WHI, nafasi zilizotangazwa ni ofisa miliki- nafasi moja, pia nafasi nyingine ni Ofisa Tehema ICT eneo la programu  kutoka Taasisi ya e-GA – nafasi sita, msimamizi wa mifumo -nafasi mbili, ofisa Tehama  mtaalamu wa miradi -nafasi mbili, ofisa Tehama msimamizi wa hifadhidata -nafasi mbili.

Eneo lingine la ajira ni ofisa Tehama mchambuzi wa biashara -nafasi moja, ofisa Tehama msimamizi wa usalama- nafasi moja, ofisa Tehama mtaalamu wa viwango na ofisa Tehema dawati la huduma -nafasi mbili.

Ajira nyingine ni ofisa Tehema mchambuzi wa takwimu- nafasi moja na kwa Chuo cha Uhasibu Arusha, nafasi iliyotangazwa ni ya ofisa Tehama idara ya usalama, mkutubi- nafasi nne kwa mikoa ya  Songea (Ruvuma), Dar es Salaam, Babati (Manyara) na Dodoma, na nafasi moja ya ofisa Mipango eneo lake la kazi Arusha. Mapokezi nafasi mbili vituo vya kazi vikiwa ni Dodoma na Arusha.

Taasisi ya Tafico, mhandisi wa majini (marine enginer)- nafasi moja, mhandisi wa mifumo ya baridi (engineer ii – refrigeration)- nafasi moja, mhandisi mitambo -nafasi moja, mtaalamu wa ufundi majini (technician ii – marine)- nafasi moja, mtaalamu wa mifumo ya baridi (technician II – refrigeration) na mtaalamu wa michoro baharini (artisan ii – marine).

Eneo lingine ni mtaalamu wa upakuaji mizigo kwenye meli (deckhand auxiliary)- nafasi moja na nahodha wa meli pia nafasi  mbili na kwa Idara ya Sanaa, nafasi zilizotangazwa ni ofisa sanaa  na ubunifu -nafasi nne, ofisa sanaa (muziki)- nafasi nne.

Nako upande wa Tawiri nafasi tatu zimetanagazwa Ofisa Utafiti II (Usimamizi wa Wanyamapori), nafasi tano ofisa utafiti msaidizi usimamizi wa wanyama pori na nafasi moja nyingine ni Ofisa Mtafiti Msaidizi (Mfumo wa Habari za Kijiografia).

Ajira nyingine zimetolewa na GPSA nafasi tano kwa maofisa usafirishaji na uagizaji, nafasi 10 kwa ofisa msaidizi wa uagizaji na usafirishaji.

Kwa NEMC, nafasi mbili zilizotangazwa ni Ofisa Usimamizi wa Mazingira II (Geolojia) Ofisa Usimamizi wa Mazingira nafasi mbili.

Ofisa Usimamizi wa Mazingira (Sayansi ya Mazingira)- nafasi nne, Ofisa Usimamizi wa Mazingira  (Usimamizi wa Wanyamapori) nafasi moja, mhandisi wa mafuta na gesi- nafasi moja na uhandisi wa rasilimali maji -nafasi moja.

Pia ipo nafasi ya uhandisi usimamizi wa viwanda -nafasi moja. Imeelezwa kuwa mwisho wa kutuma maombi hayo ni Agosti 24, 2024.

Related Posts