UJENZI WA DARAJA LA J.P MAGUFULI UPO 90% YA UTEKELEZAJI

Mwonekano wa Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) Kilometa 3.2 linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara – Sengerema – Geita kupita Ziwa Victoria na ujenzi wa barabara unganishi ya Kilometa 1.66 ambapo utekelezaji unaendelea na upo asilimia 90.

Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa shilingi Bilioni 716.3 zikijumuisha Malipo ya Mkandarasi, Mhandisi Mshauri wa usimamizi wa mradi, Fidia na Usanifu. (Picha na Wizara ya Ujenzi)    

Related Posts