CIC iliishinda CUHAS kwa pointi 78-51, katika ligi ya kikapu Mkoa wa Mwanza iliyofanyika katika uwanja wa Mirongo.
Katika mchezo huo mchezaji Bryan wa CIC aliongoza kwa kufunga pointi 24 na upande wa CUHAS, Isancho alifunga pointi 17.
Mchezo mwingine uliochezwa uwanjani hapo, Young Proffile iliishindaPlanet kwa pointi 69-51, huku Hamis wa Young Proffile akiongoza kwa point 21, kwa upande wa Planet Emmanuel alifunga point 16.
Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni Sengerema Hoopers, CUHAS, Oratorio, Profile, Young Profile, Mwanza Eagles, Planet na CIC.