HAWA HAPA WACHEZAJI WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI PFA 2023/24 – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Wachezazji sita kutoka ligi kuu ya England, Bukayo Saka, Cole Palmer, Kobbie Mainoo, Alejandro Garnacho, Joao Pedro na Michael Olise wameteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka, PFA kwa msimu wa 2023/24.

Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka yuko katika kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi mfululizo baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka jana, mwaka huu anatarajia ushindani mkali kutoka kwa Waiingereza wenzake akiwemo Cole Palmer anayeiwakilisha Chelsea, na Kobbie Mainoo wa Manchester United.

 

Wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na nyota wa Brighton and Hove Albion Joao Pedro na Alejandro Garnacho wa Manchester United na pia kiungo Michael Olise ambaye ameondoka Crystal Palace kwenda Ujerumani kujiunga na klabu ya Bayern Munich.

 

Mshindi atatangazwa rasmi katika hafla ya tuzo hizo za PFA mjini Manchester, Jumanne ijayo, Agosti 20, 2024.

Bukayo Saka  mwenye umri wa miaka 22 yuko katika kinyang’anyiro cha kuwania taji la Mchezaji Bora Chipukizi  baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka jana. Nyota huyo wa Arsenal alichangia mabao 16 na asisti tisa.

Cole Palmer mwenye umri wa miaka 22  ni miongoni mwa Wachezaji Sita Bora baada ya kuwa na  msimu bora ndani ya Chelsea akiwa amefunga mabao 22 na asisti 11.

Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 19 wa klabu ya Manchester United alimaliza msimu uliopita kwa bao la ushindi kwenye Uwanja wa Wembley kwenye Fainali ya Kombe la FA dhidi ya majirani zake Manchester City.

Mchezaji mwenzake Mainoo, Alejandro Garnacho mwenye umri wa miaka 20 pia anaingia Sita Bora baada ya kuonesha kiwango cha kuvutia kwa Mashetani Wekundu katika mechi mbili katika mashindano yote.

João Pedro mwenye umri wa miaka 22 wa Brighton pia amejumuishwa katika orodha hii baada kufunga mabao 20 katika mashindano yote.

Michael Olise mwenye umri wa miaka 22 yuko katika kinyang’anyiro baada ya kutumainiwa sana katika msimu wa 2023/24 katika klabu ya Crystal Palace. Kiungo huyo alifunga mabao 10 na kutoa asisti sita katika mechi 19 pekee.

Related Posts