Kampuni nyingi Ujerumani zinafikiria kuhamia nje ya nchi – DW – 13.08.2024

Takriban kampuni 3,300 zilishiriki katika utafiti huo. Zaidi ya nusu miongoni mwakampuni kubwa pamoja na viwandavyenye wafanyakazi zaidi ya 500, vinazingatia kuchukua hatua hiyo ya kuihama nchi na kwenda kufanya biashara zao nje ya Ujerumani.

Chama cha Viwanda na Biashara nchini Ujerumani (DIHK) kimesema sababu kubwa ya kampuni hizo kutaka kuihama nchi ni bei ya juu ya nishati na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji bidhaa, jambo ambalo linachochea matokeo mabaya kwa Ujerumani nchi iliyokuwa kitovu cha viwanda barani ulaya.

Ikitoa mfano kulingana na utafiti huo wa biashara, chama hicho cha biashara na viwanda nchini Ujerumani kimesema mwenendo wa kampuni na viwanda wa kuhamia nje ya nchi unazidi kudhihirika kila uchao.

Viwanda vya magari Ujerumani kutumia malighafi za taka

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni,kampuni nne kati ya 10 na pia viwandakwa sasa vinazingatia kupunguza uzalishaji wao nchini Ujerumani au kuhamisha biashra zao nje ya nchi kutokana na gharama kubwa za nishati.

Wanasiasa wa Ujerumani bado hawajafanikiwa kuzipa kampuni matarajio ya upatikanaji wa nishati ya uhakika na iliyo nafuu, amesema naibu Mkurugenzi wa , Achim Dercks. Amesema wakati kampuni nyingi ziliiona fursa katika mabadiliko kuelekea nishati ya kijani kwa biashara zao katika miaka ya kabla 2023, kwa maoni ya wafanyabiasha wanasema wanaona hatari zaidi kuliko fursa walizoziona awali.

Kampuni ya chipu ya Taiwan kufungua kiwanda Ujerumani

DIHK inaamini mipango inayoendelea ya kuwazuia wenye kampuni na viwanda kuhamisha maeneo ya uzalishaji, au kuhama nchi kabisa, bado inakabiliwa na maswala ya kupanda bei ya nishati na masharti katika sera ya sasa inaziongezea hasara kampuni zote za nchini Ujerumani na hivyo hazipo kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa katika ushindani wa kibiashara.

Hasa kwa kampuni na viwanda vyenye viwango vya juu vya gharama za umeme na kwa kampuni kubwa, kwa mfano za uhandisi na za uzalishaji wa bidhaa za viwandani.

Kampuni ya magari ya Volkswagen
Kiwanda cha uzalishaji magari cha Ujerumani Volkswagen Picha: Sean Gallup/Getty Images

Soma ripoti hii: Utafiti: Wanawake ni wachache mno katika nafasi za juu kwenye kampuni kubwa za Ujerumani

Chama cha Viwanda na Biashara nchini Ujerumani (DIHK)  kinataka ushuru wa umeme upunguzwe na kwamba hatua za kupunguzwa ushuru wa umeme inayotolewa na mfuko wa serikali wa ukuaji wa viwanda vya utengenezaji unapaswa kutolewa kwa kwa sekta zote.

Wanasiasa na wataalamu wa uchumi nchini Ujerumani wanasema michakato migumu kupita kiasi ya kupata ruhusa ya kujenga vituo vipya vya nishati ya upepo, ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi na kudorora kwa uwekezaji katika miundombinu ni miongoni mwa masuala muhimu ambayo nchi ya Ujerumani inahitaji kuyashughulikia.Kampuni za Ujerumani zinapanga kuwekeza zaidi barani Afrika mwaka 2023

Bei ya nishati ilipanda nchini Ujerumani baada ya Urusi kuwekewa vikwazo mwaka 2022 ilipoanza uvamizi wake nchini Ukraine. Vita vya Ukraine na janga la uviko vimeathiri mno uchumi wa dunia.

 

 

Related Posts