Rais wa Venezuela Nicholas Maduro ametoa wito kwa taifa kutumia kile alichokiita “mkono wa chuma” baada ya maandamano mabaya kupinga kuchaguliwa kwake tena mwezi Julai, kulikotajwa ndani na nje kama kichekesho.
Wakati idadi rasmi ya vifo vya maandamano hayo ikipanda hadi 25, Maduro amehimiza sheria kali kwa vurugu alizolaumu kwa upinzani, ambao unasisitiza kuwa mgombea wake Edmundo Gonzalezi Urrutia alishinda uchaguzi wa Julai 28 kwa kishindo.
Soma pia: Upinzani Venezuela waitisha maandamano ya dunia Agosti 17
Maandamano makubwa yalizuka baada ya Maduro kutangazwa rais mteule na tume ya uchaguzi, ambayo inatazamwa kama tiifu kwa utawala wake. Waangalizi wameripoti ukandamizaji mbaya wa vikosi vya usalama, ambapo zaidi ya watu 2,000 wamekamatwa.
Maduro anawalaumu Gonzalez Urrutia na kiongozi maarufu wa upinzani Maria Corina Machado, ambaye alizuwiwa kugombea urais na taasisi zinazoegemea serikali.