Michigan. Mtoto wa kike (8) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ford huko Detroit Michigan, Marekani amedaiwa kumuua mwalimu wake kwa kumpiga risasi.
Mwalimu huyo wa mazoezi ya viungo Jim Turner (56) alifariki dunia jana Agosti 12, 2024 baada ya mtoto huyo kumuua kwa kutumia bunduki ya baba yake aliyokwenda nayo shule.
Kwa mujibu wa taarifa, wakati wa darasa la mazoezi likiendelea mwalimu huyo alimpeleka mtoto huyo (jina linahifadhiwa) ofisini kwake, na dakika tatu baadaye risasi mbili zilisikika na kusababisha wanafunzi kupiga mayowe na kukimbia ukumbi wa mazoezi.
Walinzi wa shule hiyo walifika eneo la tukio na kumkuta mwalimu Turner akiwa amekufa huku mwili wake ukiwa na majeraha ya risasi kwenye paja na kifuani.
Polisi walifika muda mfupi baadaye na kumtia mtoto huyo mahabusu katika kituo cha polisi.
Mwanafunzi huyo amedai kwamba mwalimu Turner alikuwa akimgusa sehemu zake za siri na kumtisha ikiwa atamwambia mtu yeyote, kwa hiyo akiwa na hofu na kukata tamaa, alichukua bastola ya baba yake aliyokuwa akiificha chini ya godoro na kuja nayo shuleni ili kujilinda dhidi ya mwalimu huyo.
Picha za usalama kutoka shuleni hapo zilionesha Turner akimpeleka mtoto huyo ofisini kwake mara kwa mara.
Kutokana na tukio hilo, wazazi wa mtoto huyo wanatarajiwa kukabiliwa na mashtaka kuhusiana na kifo cha Turner.
Endelea kufuatilia Mwananchi.