Polisi Tanzania wapata mafunzo Kenya wa ahidi kuboresha huduma kwa wateja

Jeshi la Polisi Tanzania katika kuhakikisha linaendelea kujiimarisha katika kila sekta mbalimbali awamu hii wameendelea na mafunzo jijini Nairobi kujifunza na kuona namna bora ya kuwainua kiuchumi askari Pamoja na familia zao kwa kupata fursa ya mafunzo na namna bora ya kuendesha sacoss ya Jeshi la Polisi Nchini Tanzania.

Akiongea leo Jijini Nairobi mara baada ya mafunzo hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Usalama wa raia Saccos Kamishna wa Utalawa na Menejimenti ya raslimali watu CP Suzan Kaganda amesema kuwa wamejifunza vitu vingi ambavyo vina tija katika uendeshaji wa saccos yao huku akiweka wazi kuwa wanakwenda kuboresha huduma baada ya mafunzo hayo.

CP Kaganda ameongeza kuwa kuwepo kwao Nairobi imekuwa ni fursa na hamasa ya kujifunza masuala yahusuyo saccos ambapo amewapongeza saccoss ya Polisi Nchini Kenya namna ambavyo imeonyesha viwango bora katika kutoa huduma huku akiipongeza kwa kushika nafasi za juu katika kutoa huduma bora za chama hicho.

Nae David Kagogo ambaye ni Naibu mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi nchini Kenya SACCO amewashukuru askari hao kutoka Tanzania kufika na kujifunza namna ambavyo nchi hiyo inavyofanya kazi katika chama hicho huku akiwaomba kuyachukua mafunzo hayo kikamilifu ili kuongeza ufanisi na maarifa katika utendaji kazi ndani ya saccos ya Polisi Tanzania.

Related Posts