WYDAD CASABLANCA KUMSAJILI PERCY TAU – MWANAHARAKATI MZALENDO

Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco inataka kumsajili nyota wa klabu ya Al Ahly ya Misri na timu ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, Percy Tau mwenye umri wa miaka 30.

Mjumbe wa bodi ya klabu ya Wydad Casablanca, Saad Al-Dreib amethibitisha ilo kwa kusema “Mchezaji kama Percy Tau, ni miongoni mwa (wachezaji) wengine, bila shaka ni mtu ambaye tunataka kumsajili.”

Wydad Casablanca kwa sasa ipo chini ya kocha Rhulani Mokwena aliyekuwa kocha wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Baadhi ya vyanzo vya habari kutoka nchini Morocco vinasema kama mambo yataenda vizuri nyota huyo atapewa mkataba wa hadi mwaka 2027.

#KonceptTvUpdates

Related Posts