AMUUA JIRANI YAKE KISA ANA KOROMA KWA SAUTI KUBWA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mwanamume mmoja wa Philadelphia nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha kwenda jela baada ya kukiri kosa la kumuua bila kukusudia jirani yake kufuatia mzozo ambao mamlaka zinasema ulikuwa ni kuhusu kukoroma kwa sauti kubwa.

 

Christopher Casey (56) anayeonekana kwenye picha, amehukumiwa wiki iliyopita kwenda jela kwa miezi 23 baada ya kukiri shtaka la kuua bila kukusudia na kumiliki silaha aliyoitumia katika uhalifu huo.

 


Imeelezwa kuwa Casey alisababisha kifo cha Robert Wallace mwenye umri wa miaka 62 ambaye nyumba zao zilikua zimeshikana na kutenganishwa na ukuta mmoja ambapo ukaribu huo ulisababisha kukoroma kwa Robert kusikike hadi kwa jirani yake huyo.

Wallace alipatikana umbali wa futi 50 kutoka kwenye nyumba yake akiwa na jeraha la kuchomwa kisu wakati Polisi walipofika.

Related Posts