Hilmy kuiwakilisha Tanzania Paralimpiki 2024

Na Winfrida Mtoi

Mtanzania Hilmy Shawwal ni mchezaji pekee anayetarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya michezo ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu(Paralimpiki Paris 2024), itayoanza  Agosti 28 hadi Septemba 8, 2024 nchini Ufaransa.

Hilmy ambaye anaishi  Uingereza, atashindana katika  mbio za Viti-Mwendo Daraja la T54.

Mchezaji huyo amefanikiwa kupata nafasi hiyo ya pekee kupitia WildCard baada  ya kuwa  miongoni mwa wachezaji bora kwa watu wenye ulemavu barani Ulaya hasa Uingereza, hivyo Kamati ya  Paralimpiki Tanzania (TPC), kumpitisha kuwakilisha nchi.

Kwa mujibu wa baba mzazi wa mchezaji huyo, Faria Shawwal, mwanaye ameshiriki mashindano mengi ya Kimataifa na ana matumaini ya kufanya vizuri Paralimpiki.

“Hilmy ni kijana ambaye hakati tamaa, akitaka kitu lazima kiwe. Ameshiriki mashindano mbalimbali hapa Uingereza kama World Championship na amepata medali tofauti tofauti katika mashindano hayo,” ameeleza Shawwal.

Akizungumzia historia ya mtoto wake huyo, amesema alizaliwa nchini Uingereza akiwa na ugonjwa wa mgongo wazi na alianza kushiriki michezo tangu akiwa chekechea na alipofikisha umri wa  miaka tisa tayari alianza kucheza mpira wa kikapu lakini haikuwa chaguo lake.

Related Posts