Klabu ya KMC imetangaza kumrejesha kikosini kiungo Awesu Awesu aliyekuwa akiichezea timu hiyo msimu uliopita kabla ya kuelezwa amesajiliwa na Simba na kutangazwa Julai 17, 2024.
Licha ya kutangazwa Simba kama mchezaji mpya atakayekitumikia kikosi hicho cha wekundu kwa msimu wa 2024\25, usajili huo ulikuwa na dosari, kwani KMC ilidai bado ana mkataba na wanakino boys kwa mwaka mmoja, hivyo hawautambui usajili wa kwenda Simba.
Muda mchache uliopita KMC kupitia ukurasa rasmi wa klabu wa mtandao wa Instagram wametupia picha ya Awesu Awesu, ikiisindikizwa na ujumbe ‘welcome back’ ukiwa na maana ya karibu tena.
Hata hivyo, imesalia siku moja tu kufungwa kwa dirisha kubwa la usajii la msimu wa 20234/25 linalotarajiwa kufungwa kesho Agosti 15 saa 6:00 usiku.