Watu wasiopungua 575 wameshatakiwa, huku mahakama zikiendelea kuwashughulikia walioshiriki fujo hizo zilizoikumba miji kadhaa ya England na Ireland Kaskazini, kufuatia vifo vya wasichana watatu waliochomwa kisu Julai 29.
“Vikosi kote nchini hivi sasa vimekamata watu zaidi ya 1,000 kuhusiana na vurugu za hivi karibuni na fujo,” Baraza la wakuu wa polisi ya taifa, NPCC, lilisema kupitia mtandao wa X.
Fujo hizo za wafuasi wa itikadi kali zilifuatia taarifa za upotoshaji kuhusu utambulisho wa mshukiwa wa shambulio hilo la kisu, ambapo pia watu kadhaa wamefungwa jela kwa kueneza chuki mtandaoni katika siku za karibuni.
Soma pia: Mfalme Charles III azungumzia maandamano ya vurugu Uingereza
Mahakama ya Uingereza inapitia kwa haraka kesi za mahakama na kutoa hukumu za vifuno virefu baada ya machafuko kutulia kabla ya wikendi na serikali imeapa kuwachukulia hatua kali waliohusika.