SIMBA YAONYWA KUMRUBUNI AWESU AWESU – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa onyo kwa Simba SC kwa kumrubuni mchezaji wa KMC Fc Awesu Awesu na kumtangaza kuwa mchezaji wao katika mitandano yake ya kijamii bila kufuata utaratibu.

Taarifa ya TFF imefafanua kuwa uamuzi huo umefikiwa katika kikao chake cha tarehe Agosti 10, 2024 ikasikiliza pande zote mbili (KMC FC na Simba SC) kabla ya kuamua kuwa Awesu Ali Awesu ni mchezaji halali wa KMC FC, na kama Simba SC inamuhitaji mchezaji huyo izungumze na klabu yake.

“Malalamiko ya klabu yako ni kuwa Simba SC imemrubuni mchezaji Awesu Ali Awesu, na kumtangaza kuwa mchezaji wao katika mitandano yake ya kijamii bila kufuata utaratibu wakati suala lake likiwa bado halijatatuliwa”

Hata hivyo Kamati ya TFF imekiri kuwa haikupata ushahidi wowote kutoka KMC FC kuwa Simba SC ilimrubuni mchezaji huyo wa zamani wa Madini FC.

Related Posts