Watoto Sengerema wapata mafunzo | Mwanaspoti

MAKOCHA wa mpira wa kikapu nchini wanaendelea kuendesha program za mafunzo ya mchezo huo kwa watoto, huku kwa upande wa Mwanza, Kocha wa mkoa huo, Benson Nyasembwa amesema Beka sports consultant ya mkoani humo, iliendesha mafunzo hayo Wilaya ya Sengerema.

Nyasebwa aliiambia Mwanasposti mafunzo hayo yaliwahusisha watoto wa kuanzia umri wa miaka 6 hadi 15, lengo likiwa ni kuwahamasisha waupende mchezo huo.

“Kwa kweli tulifanikiwa na watoto hao kutuomba  turudi wakati mwingine,” alisema Nyasebwa.

Alisema mafunzo hayo yaliendeshwa na makocha wa nne ambao ni Elineema Mbwambo, Elizabeth Hambo, Pily pamoja na yeye mwenyewe.

Related Posts