RAISI wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ally Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zote kwa ujmla wake zinazingatia haki na Uhuru wa kuabudu kama msingi muhimu wa kuleta umoja kwa Watanzania na kudumisha Amani.
Dkt Mwinyi amesema hayo mapema leo hii Jijini Dodoma Agost 16,2024 wakati akifunga Mkutano wa 8 wa Baraza Kuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) 2024, uliofanyika Jijini hapa.
Nakuongeza kuwa Serikali hizo zitaendelea kusimamia misingi hiyo kwa manufaa ya Watanzania wote na Amani ya Nchi.
“Napenda nikuhakikishie kuwa Serikali zetu zote mbili zinazingatia haki na uhuru wa kuabudu kama msingi muhimu wa kuleta umoja wa Watanzania na kudumisha Amani”.
“Kwa mnasaba huo napenda nikuahidi Baba Askofu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaendelea kusimamia misingi hiyo kwa manufaa ya Watanzania wote na a I ya Nchi yetu”.
Aidha Rasi Mwinyi amesema Serikali zote zinadhamini kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Taasisi za Dini katika kuhubiri amani na kuhudumia jamii katila sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu,Maji safi na Kufusa watu wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu na Wazee.
“Aidha Serikali zetu zinadhamini kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi za Dini katika kuhubiri amani na kutoa huduma za kijamii katika sekta ya Elimu,Afya, Maji safi na salama na kusaidia watu wenye mahitaji maalum wakiwemo watu wenye ulemavu na wazee”.
Sambamba na yote ameahidi kuendelea kutatua changamoto zinakabili Taasisi za dini ili zifanye kazi kwa ufanisi na kuendelea kulinda na kudumisha umoja wa Watanzania ili waishi kwa kushirikiana na kuheshimiana.
“Napenda niwaahidi kwamba tutaendelea kuwapa ushirikiano katika kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazozikabili Taasisi za dini ili ziweze kutekeleza majukamu yao kwa ufanisi zaidi”.
“Aidha Serikali inatambua umuhimu wa umoja, kwahivyo tutaendelea kuchukua kila hatua kuhakikisha tunalinda na kudumisha umoja wa Watanzania na kuhakikisha wananchi wote wanaishi kwa kushirikiana na kuheshimiana”.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa hilo la TAG Dkt Barbanas Mtokambali ametumia fursa hii kumpongeza Dkt Mwinyi na Serikali ya Mapinduzi kwa kuonesha msimamo madhubiti kwa vitendo wenye kuleta usawa wa haki ya kikatiba katika uhuru wa kuabudu pale alipo laani vitendo vya unyanyasaji katika maeneo mbalimbali huko Zanzibar dhidi ya watu wa imani tofauti pamoja kuhimiza hali ya kuvumiliana na kustahimiliana katika taratibu za ibada za imani za katika made madhehebu ya dini tofauti ila mradi pasivunjwe sheria.
“Aidha tunakupongeza sana wewe Raisi Mwinyi na Serikali ha Mapinduzi kwa kuonesha msimamo madhubuti wenye kuleta usawa na haki ya kikatiba katika uhuru wa kuabudu pale ulipo laani vitendo vya unyanyasaji katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar dhidi ya watu wa imani tofauti pamoja na kuhimiza hali ya kuvumiliana na kustahimiliana katika taratibu za ibada za imani za kidini katika madhehebu ya dini tofauti ili mradi pasivunjwe Sheria. Hili tymelipokea kwa moto mkunjufu sana kwa hakika kauli yako na msimamo wako imezidi kuimarisha amani ya Nchi”.
“Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Serikali kwa vyombo vya habari,Walaka wa SMZ tarehe 30 March 2024 kuhusu uvumilivu wa kidini. Na Inawezekana tunapoongea uvumilivu wa kidini duniani basi Zanzibar mpo juu sana na Ikumbukwe kuwa hata ukristu wakati umeingia ukand huu wa Afrika Mashariki uliingilia Zanzibar dio maana bado kuna mabaki ya majenjo ya kale yaliyotumika kama Makanisa”.
Huu ni Mkutano wa nane wa Baraza Kuu TAG 2024 uliowakutanisha viongozi zaidi ya elfu 6 wa dini kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ya chini ya Kanisa la TAG.