Kijana Abdul (30) afikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kulawiti na kuwabaka watoto 7 Bukoba.

Kijana Abdul Suleiman maarufu kama Mzee Abdul mwenye miaka 30 mjasiliamali mkazi wa kata ya Kahororo iliyopo manispaa ya Bukoba amefikishwa mahakamani kwa tuhuma ya ubakaji na ulawiti kwa watoto 7 wanaosoma shule ya msingi katika manispaa hiyo ya Bukoba.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa leo August 14 katika mahakama ya Wilaya Bukoba iliyopo Mkoani Kagera huku akikabiliwa na kesi mbili,ambapo shitaka la kwanza lenye namba 22890 ya mwaka 2024 ikiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Bukoba Frola Kaijage,anashitakiwa kwa kosa la ubakaji wa mtoto wa darasa la tatu mwenye miaka 9.

Wakili wa Serikali Evaresta Kimaro ambaye anasimamia kesi hiyo amesema kuwa mshitakiwa huyo tayari amesomewa hoja za awali na shahidi mmoja amesikilizwa japo mtuhumiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande mpaka August 28 mwaka huu wa 2024 ambapo kesi yake itaendelea kusikilizwa.

Aidha mshitakiwa Abdul Suleiman maarufu kama Mzee Abdul amefikishwa katika mahakama hiyo ya Wilaya ya Bukoba kwa kesi ya pili yenye namba 22889 ya mwaka 2024 kwa makosa mawili ya ubakaji na ulawiti kwa watoto sita ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi iliyopo manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

 

Related Posts