MASHETANI WEKUNDU UWANJANI LEO KUIFUNGUA EPL

KLABU ya Manchester United leo itashuka dimbani kuikaribisha klabu ya Fulham katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Uingereza ambao utachezwa katika dimba la Old Trafford.
Ni msimu mwingine wa kujiuliza kwa klabu ya Manchester United juu ya ubingwa wa ligi ya Uingereza ambao mabingwa hao mara (20) wa ligi hiyo wameukosa kwa takribani miaka kumi sasa, Ambapo kipimo cha kwanza kitakua Fulham pale kwenye dimba la matofali ya kuchoma.
Mchezo wa leo unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa kwani klabu ya Fulham pia ni moja ya timu ambazo zimekua na ubora kwenye ligi kuu ya Uingereza, Wakiwa wameongeza wachezaji wenye ubora kwenye kikosi msimu huu.
Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.
Ikumbukwe mara ya mwisho klabu ya Fulham kufika katika dimba la Old Trafford walifanikiwa kushinda kwa mabao mawili kwa moja, Hivo mchezo wa leo sio mwepesi kutokana na kilichofanywa mara ya mwisho na Fulham walipokutana tena katika uwanja wao wa nyumbani.

Related Posts