DODOMA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga amepokea Jendwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo za Mwaka 2024 katika Mkutano wa Kumi na Tano, Kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimewasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.
Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma ambapo amesema mafanikio ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) yanatokana na ushirikiano ambao umekuwa ukitolewa na Kamati ya Bunge ya Sheria ndogo.
“Naomba niwahakikishie kamati; nimepokea jedwali hili na tutawasilisha kwa Wizara zinazohusika ili zije zilete majibu, naomba tuendele kupata ushirikiano wakati wizara hizo zitakapokuja kuwasilisha,” alisema Naibu Waziri Ummy.