RC akemea Beach boy kunyang’anya wake za watalii ZNZ

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rc Ayoub Mohammed Mahamoud amekasirishwa na kukemea kwa tabia iliokisiri kwenye fukwa za Bahari za kusini na Zanzibar kwa Baadhi ya Ma Beach Boys kupora wake wa Watalii wanaoingia nchini kwa shughuli za kitalii jambo ambalo limekua likikasirishwa watalii waingia nchini

Rc Ayoub ameyasema hayo kwenye semina ya waongoza watalii na Beach Boys ikiwa inaelekea tamasha la kizimkazi festival linalotarajiwa kudhuriwa na watalii na wenyeji katika Mkoa wa kusini ,ambapo mkuu wa mkoa amebainisha kuna changamoto ambazo zimekua zikisababishwa na watu wasiofata utaratibu na kwamba matatizo yanayojitokeza kwa beach boys yatakwenda kua mwisho

” Wale ambao bado wataendelea kukaidi utaratibu uliotolewa hapo sasa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ,hatutomvulia yule atakaedhoofisha uchumi wetu kwa kuleta utalii usiofata utaratibu ,watanzania tunaowaita beach boys wamekua na tabia ya kunyanganya wake wa watalii jambo ambalo linapelekea watalii kuichukia nchi yetu na ndio maana nimelikemea hilo ili wale ambao wenye tabia hizo tuwaondoa sababu watakua wamekosa vigezo katika mkoa wetu —asema Rc Ayoub”

Related Posts