Sababu Onyango kutotangazwa Dodoma Jiji

IMEELEZWA kwamba sababu ya uongozi wa Dodoma Jiji  kuchelewa kumtangaza beki Joash Onyango ni kutaka mchezaji huyo amalizane kabisa na Singida Black Stars aliyoichezea msimu uliopita.

Onyango bado ana mkataba na Singida Black Stars, hivyo Dodoma Jiji inataka imchukue kama mchezaji huru na siyo kucheza kwa mkopo kama ilivyokuwa awali.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Patrick Semindu amesema imekuwa vigumu kumtangaza beki huyo wa zamani wa Simba kabla hajamalizana na timu yake.

“Kila kitu kikiwa tayari itakuwa rahisi sisi kumtangaza, kwani tunaamini ni suala la muda na hakuna kitu kinashindikana kwa kukaa mezani na kuyajenga.”

Onyango 2024/25 itakuwa msimu wake wa tano katika Ligi Kuu Bara kwani mara ya kwanza alijiunga na Simba 2020/21 kabla ya kutua Ihefu iliyobadili jina na kuwa Singida Black Stars.

Related Posts